Isaiah 65:5-7

5 awasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie,
kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’
Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,
ni moto uwakao mchana kutwa.

6 b“Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:
sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;
nitalipiza mapajani mwao:
7 cdhambi zenu na dhambi za baba zenu,”
asema Bwana.
“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima
na kunichokoza mimi juu ya vilima,
nitawapimia mapajani mwao
malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”
Copyright information for SwhNEN